Katika kitabu hiki Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi anauzungumzia hatua kwa hatua, Mzizi wa kwanza wa Uislamu (Umoja wa Mungu). Anaanza kwa kuzungumzia kihoja sababu zitufanyazo tuamini kuwepo kwa Mungu, kisha anazipinga hoja za wanasayansi zipingazo kuwepo kwa Mungu; anatoa hoja za imani yetu (ya Umoja wa Mungu) na anamalizia kwa “Maana ya Umoja wa Mungu.”